(255) 0678 393 950, 0753559833

Kanuni

KANUNI NA MWONGOZO WA MASHINDANO YA KUJENGA MWILI YA MR. TANZANIA.

(1) Washindani ambao ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kuandikishwa uraia bila kujali dini, rangi au makabila wataruhusiwa kushiriki shindano la Mr. Tanzania, pia washiriki toka katika GYM na Klabu za mazoezi ya kujenga mwili wenye viwango vya ubora wa ujenzi wa hali ya juu watapata nafasi ya kushiriki shindano la Mr. Tanzania.

(2) Kila mshindani wa shindano la Mr. Tanzania anatakiwa kujifunza na kufahamu kwa ufasaha hatua saba za msingi za utunishaji misuli ambazo ni:-

  1. Front double biceps
  2. Rear double biceps
  3. Front lat spread
  4. Rear lat spread
  5. Side chest to the left right – Quarter turn
  6. Triceps flex with left side and right – Quarter turn
  7. Abdominal flex with legs

(3) Mashindano ya Mr. Tanzania yataendeshwa na kutolewa maamuzi ya matokeo ya washindi kwa kufuata viwango vinavyoendana na viwango vya kimataifa vya maamuzi kwa sababu mshindi wa shindano la Mr. Tanzania atakuwa ni balozi wa nchi katika mashindano ya kimataifa ya (Mr. World), (Mr. Universe), (Mr. Africa).

(4) Utumiaji wa madawa ya aina yeyote hauruhusiwi kwenye shindano la Mr. Tanzania. Yeyote atakaegundulika anatumia madawa au madawa yeyote yaliyokatazwa ataondolewa kwenye mashindano ya Mr. Tanzania haraka sana na atafungiwa kwa kipindi kirefu toka kwenye mashindano

(5) Mshiriki yeyote ambae atahisiva kutumia Madawa ya aina yoyote au yaliyo pigwa marufuku atachukuliwa haraka kwa ajili ya vipimo vya damu na mkojo kabla au baada ya shindano, na hatakiwi kukataa kwa hilo. Pingamizi lolote juu ya vipimo kuhusu utumiaji wa dawa litachukuliwa kama mwenye hatia ya utumiaji na itabidi kurudisha taji aliloshinda na litakabidhiwa kwa mshindi wa pili

(6) Washindani wa shindano la Mr. Tanzani body building wana haki ya kushindana mara mbili au tatu kugombania taji lenye hadhi la Mr. Tanzania. Mr. Tanzania kama bingwa mtetezi ana haki ya kutetea taji lake mara tatu tu kwa mfululizo baada ya hapo hatoruhusiwa tena kugombea

(7) Washiriki wote kutoka mikoa yote ya tanzania watapewa kipaumbele sawa na watashindana kwa moja mmoja kwa heshima mchezo huu.

(8) Uamuzi wa Waamuzi uliofanywa katika shindano ni wa mwisho hakuna kupinga matokeo kwa kipindi cha mwaka uliofanyika shindano pia haiwazuii washiriki walioshindwa kupaza sauti zao kwa kamati ya mashindano mr. Tanzania jinsi gani shindano lilivyo amriwa ndivyo sivyo, lakini iwapo baada ya uchunguzi ikaonekana kuwa kuna makosa ya uamuzi wa mshindi waliofanya uzembe huo hawatarudi kukaa katika meza ya waamuzi katika mashindano ya mwaka unaofuata.

(9) Mashindano ya Mr.Tanzania yatashindaniwa kwa kufuata madaraja ya ushindani kuanzia uzito mwepesi(60_65kilo)Uzito mwepesi wa kati(65-69)Uzito wa kati(70-75)Uzito wa juu mwepesi(178-85) na pia Uzito wa juu(90)na kuendelea zaidi ya hapo,Mshindi wa kwanza ,wa pili na wa tatu toka katika kila daraja watachuana kumchagua mshindi wa jumla taji la Mr. Tanzania na mshindi ndiye atakae kuwa Mwakilishii wa nchi katika mashindano ya Mr. Afrika,Mr.World na Mr. Universe.

(10) Mshindi wa shindano la Mr. Tanzania atakuwa balozi mzuri wa mchezo wa kujenga mwili,pia Balozi wa Wadhamini waliodhamini shindano .hivyo basi washindi wa shindano la Mr. Tanzania wanatakiwa kuishi maishi ya utiifu na unyenyekevu kwa jamii.

(11) Washiriki wote wa shindano la Mr. Tanzania tangu wakarti wa mchujo wa awali hadi wakati wa usiku wa fainali ya yenyewe ya Mr.Tanzania waatatakiwa kuvaa vazi maalum fupi mfano wa bukta ya kubana ambalo litatolewa na shirikisho la kujenga mwili la Tanzania(TBBF)na pia litakuwa na nembo ya mdhamini wa shindano.

(12) Pamoja na kwamba waamuzi wa shindano la Mr. Tanzania wanachaguliwa na kamati ya mashindano ya Mr. Tanzania lakini pia Mwangalizi toka Baraza La Michezo La Taifa atakuwepo katika kuangalia jinsi zoezi zima la kumchagua mshindi linavyoendelea, Shindano ili kupata mshindi litatolewa maamuzi na Waamuzi sita.

(13) Tuzo ya Mr Tanzania Handsome itakwenda kwa Mshindani ambae ataonyesha umbo zuri,uwiano wa misuli ulio sawa,ikichanganyika na mwonekano wa mwili wote , mshiriki atatakiwa kuwa na mwonekano wenye hadhi na na kujiamini   kwa uwezo wa kiwango cha juu anapokuwa jukwaani, Kujiamini kuwe kwa uwazi zaidi,pia watapigiwa kula kupitia mtandaoni na wananchi wakati wa shindano litakapokuwa linaendenlea

(14) Mr. Tanzania photogenic bodybuilder imelengwa kwa ajili ya wanaume wanaofanya mazoezi ya kujenga mwili gym kwa kutumia vifaa vya uzito wa kawaida ,kula kwa kufuata mpangilio mzuri wa chakula chenye afya ,lakini pia ambao umejengeka kimichezo na wenye kuvutia,muonekano mzuri wa uso,misuli iliyojipanga vyema,ngozi safi yenye kupendeza,mwenye uso wenye muonekano safi wa picha,pia shindano hili litaamuliwa pia kwa washiriki kupigiwa kula mtandaoni kwa uchaguzi wa kura za wananchi.

(15)  Washiriki wanatakiwa kuepukana na mienendo mibaya na kufanya mambo kwa heshima ili kutolipa jina baya shindano kwa kutoa maelezo yasiyo sahihi mbele ya waandishi au vyombo vya habari bila ya kuwasiliana na kamati ya mashindano ya Mr.Tanzania

(16) Washindi wa mashindano ya Mr. Tanzania, Mr. Africa, Mr. Unirvese, Mr. Handsome na Mr. Photogogenic wote watakuwa chini ya uangalizi na uongozi wa TBBF wakishirikiana na PILI PILI ENTERTAIMENT kwa muda wa miaka mitatu (3). TBBF na Pili Pili watawaandalia mafunzo, kuwapatia matangazo ya biashara na mapato halali yatakayopatikana kwa ajili ya kazi hiyo ya matangazo na shughuli nyingine yatagawanywa kwa uwianao wa 60%:40%, wakati TBBF watapata 60% na mshindi atapata 40% ya mapato.

(17) Ikitokea kukawa na upungufu wa washiriki,usimamizi una haki ya kuhairisha mashindano.

Kanuni na mwongozo wa mashindano ya Mr. Tanzania ndiyo msingi unaoongoza na kutawala mfumo mzima wa mchezo wa kujenga mwili Tanzania, yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni na mwongozo huu ataenguliwa kushiriki shindano la Mr. Tanzania.