MASHARTI:
SHERIA ZA MCHEZO:
- Washiriki wote wa Mr. Physique na Miss. Fitness wanatakiwa kuwasili Serene Beach Resort (Zamani – Bellinda Hotel) karibu na Jangwani Sea Breeze, Mbezi Dar es Salaam siku ya 26/11/2019 saa 1:00 asubuhi na washiriki wa Mr.Tanzania watatakiwa kuwasili siku 28/11/2019 saa 1:00
- Unaweza kujifunza aina tofauti za poses kama zitakavyoonekana kwenye mitandao yetu ya kijamii Instagram/Facebook/YouTube account “tanzaniabodybuilding” au youtube video ya chaneli ya kimataifa.
- Utafudishwa zaidi kupose na wataalamu wetu kwenye kambi ya mashindano.
- Hakuna mshiriki atakayeruhusiwa kutoka nje ya kambi pindi atakapochaguliwa kutoka kwenye mchujo wa awali kuanzia 26/11 hadi 29/11 kwenye hitimisho la mashindano.
- Washiriki watakaoshindwa kufuata sheria wanaweza kutolewa na kufungiwa kuonekana kwenye mashindano hayo na mengine yatakayo fuata .
- Hakuna mshiriki yeyote atakaye ruhusiwa kuhojiwa na chombo chochote cha mawasiliano bila ruhusa ya mdhamini kwa kipindi chote cha kambi ya mashindano .
- Washiriki watapata huduma za malazi kwa kushirikiana kwa kipindi chote cha kambi ya mashindano.
- Kufuata sheria za shindano-uamuzi wa mwisho utafanywa na mdhamini .
- Washiriki wanawake /wasichana wanatakiwa kuvaa sports bra na sports tight shorts .
- Physique watavaa kabtula kwa ajili pose.
- Hakuna mwanafamilia , rafiki , mchumba atakaye ruhusiwa kwenye kambi ya mashindano.
- Washiriki wote watapatiwa kibali cha mtu MMOJA wa familia kuja kushuhudia fainali katika hoteli ya Hyatt regency
KUSTAHIKI:
- Mashindano haya ni ya wazi kwa wanamichezo wote.
- Physique ni kwa wanamichezo wote kuanzia umri wa miaka 18 mpaka 35.
- Fitness ni kwa wanamichezo wote kuanzia umri wa miaka 18 mpaka 45.
- Tanzania watunisha misuli kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea.
- Kutakuwa na aina tatu za uzito kwa Mr. Tanzania.
- Kila mshiriki anaruhusiwa kuingia kwenye aina moja ya ushiriki.
HAKUNA MUINGILIANO WOWOTE UTAKAO RUHUSIWA KATI YA BODYBUILDING NA PHYSIQUE.
Mshiriki anaweza kubadilisha aina ya ushiriki pale atakapo wasili kambini kabda ya mchujo wa awali kuanza.
MADARAJA YA UZITO
Men’s Body Builder: uzito mwepesi.55Kilo – 69 Kilo | uzito wa kati. 70 Kilo – 79 Kilo | uzito wa juu.80kilo
Men’s Mr. Physique: Uzito wowote
Women’s Physique: Uzito wowote
TUZO: Tuzo zote zitatolewa kwa washindi wote na zawadi za kifuta jasho kwa washiriki wengine ambao hawatashinda.
Kwa habari zaidi za zawadi tembelea tovuti yetu www.tzbbf.org
MUDA WA POSE: Muda wa pose usizidi sekunde sitini kwa onyesho la mwisho kwa kila mshiriki.
VAZI LA POSE: Mavazi ya pose yanaweza kuwa na rangi moja au mchanganyiko.
MAHITAJI:
Idadi ya mavazi yanayohitajika kwa washiriki kuwa nayo kipindi cha mashindano:
- Stylish Suits kwa wanaume (Aina: Mr. Physique na Mr. Tanzania), Vazi la heshima kwa wanawake.
- Vazi la ubunifu la kitamaduni ( Kwa aina zote za washiriki)
- Suruali (ya blue na nyeusi) (Kwa aina zote za washiriki)
- Nguo ya Juu (kama singlet inashauriwa kuwa nyeusi)( Kwa aina zote za washiriki)
- Nguo ya kulalia (Kwa aina zote za washiriki)
- Vazi kwa wasichana/wanawake (kaptula , sport bra(Wanawake/wasichana) ,kabtula kwa wanaume , singlet ,Viatu, Leso)
- Mavazi ya kawaida (Kwa aina zote za washiriki)
- Vazi rasmi kama itatokea kuna mkusanyiko wa kijamii (Kwa aina zote za washiriki)
Ubao wa alama/Sheria kwa Mr. Physique:
- Popular – 10%
- Extreme Fitness – 10%
- Top Model Competition – 10%
- Beach Wear – 10%
- Suit – 10%
- Poses(Front & Rear Double biceps and Chest, Abdominal Flex and Legs.) – 10%
- Preliminary Questions – 20%
- Final Question – 20%
Total – 100%
Ubao wa alama/Sheria kwa Ms. Fitness :
- Popular – 10%
- Extreme Fitness – 10%
- Top Model Competition – 10%
- Beach Wear – 10%
- Smart Formals – 10%
- Poses(Front & rear double biceps, Abdominal Flex and Legs) – 10%
- Preliminary Questions – 20%
- Final Question – 20%
Total – 100%
Ubao wa alama/Sheria kwa Mr. Tanzania
- Front and Rear Double Biceps – 10%
- Chest Left and Right – 10%
- Quarter turns and Side biceps – 10%
- Front Lat Spread – 10%
- Rear Lat Spread – 10%
- Abdominal Flex with legs – 10%
- The most Muscular Pose – 10%
- Suit – 10%
- Final Question – 20%
Total – 100%
Ratiba ya Matukio
Mr. Physique na Miss Fitness TAREHE: jumanne,26/11/2019
Mahali: Serene Beach Resort (zamani– Bellinda Hotel) karibu na Jangwani Sea Breeze , Mbezi Dar es Salaam.
MUDA | TUKIO |
1:00 -03:30 asubuhi | Usajili |
4:00 -8:00 mchana | Mchujo (Mr. Physique na Miss. Fitness) |
8.00 – 9:00 mchana | Chakula cha mchana kwa waliopita na Lunch box kwa wasiochaguliwa. |
9:00 – 10:00 jioni | Kuonyeshwa sehemu za malazi kwa waliochaguliwa . |
12:00 -2:00 usiku | Maelekezo kwa washiriki (walimu, wanamitindo & uongozi) |
2:00 – 3:00 usiku | Chakula cha jioni |
3:00 -4.00 usiku | Kipindi cha mitandao ya kijamii Mr. and Miss. Popular Contest. |
Mr. Physique na Miss Fitness Date: Jumatano,27/11/ 2019
Mahali: Serene Beach Resort (zamani – Bellinda Hotel) karibu na Jangwani Sea Breeze, Mbezi Dar es Salaam.
MUDA | TUKIO |
1:00 -2:00 asubuhi | Kifungua kinywa – Sehemu: Hotelini |
5:00 – 8:00 mchana | Kwa Mr. Physique (Shindano: Beach Body Top Model and Extreme Fitness)
Sehemu: Ufukweni |
8.00 – 9:00 mchana | Chakula cha mchana, Sehemu: Ufukweni |
9:00 – 12:00 jioni | Chai na vinywaji kwa Miss. Fitness (shindano : Beach Body, Top Model and shindano la Extreme Fitness )
Sehemu: Ufukweni |
12:00 – 2:00 usiku | kupumzika – Sehemu: Hotelini |
2:00 -3:00 usiku | Chakula cha usiku – Sehemu: Hotelini |
3:00 – 4.00 usiku | Kipindi cha mitandao ya kijamii kwa Mr. and Miss. Popular Contest. |
Mr. Physique Na Miss Fitness Tarehe: Alhamisi,28/11/2019
Mahali: Serene Beach Resort (zamani – Bellinda Hotel) Karibu na Jangwani Sea Breeze , Mbezi Dar es Salaam.
MUDA | TUKIO |
1:00 – 2:00 Asubuhi | Kifungua kinywa – Sehemu: Hotelini |
2:00 -8:00 Mchana | Mazoezi Mr. Physique (Beach & Top Model mafunzo na mazoezi na upimaji na upigaji picha)
Miss. Fitness (Beach & Top Model mafunzo na mazoezi na upimaji na upigaji picha) Sehemu: Hotelini |
8.00 -9:00 mchana | Chakula cha mchana, Sehemu: Hotelini |
11:00 – 2:00 usiku | Mazoezi ya vitendo na upigaji picha |
Mr. Tanzania 2019 Tarehe: Alhamisi,28/11/2019
Mahali: Serene Beach Resort (zamani – Bellinda Hotel) karibu na Jangwani Sea Breeze , Mbezi Dar es Salaam.
MUDA | TUKIO |
1:00 – 3:30 asubuhi | Usajili – Sehemu: Hotel |
4:00 – 5:00 asubuhi | Mkutano na wahadishi wa habari |
6:00 -8:00 mchana | Mchujo wa awali |
8.00 – 8:30 mchana | Chakula cha mchana – Sehemu: Hotelini |
8:30 – 12:00 jioni | Mchujo wa awali unaendelea |
12:30 -1:30 jioni | Mwelekeo |
Mr. Tanzania 2019, Mr. Physique Na Miss Fitness Tarehe: Ijumaa,29/11/2019
Sehemu: Hyatt Regency – Dar es Salaam.
MUDA | TUKIO |
2:00 – 4:00 asubuhi | Kifungua kinywa |
4:00-8:00 Mchana | Mazoezi ya jukwaa |
8.00 -9:00 Mchana | Chakula cha mchana |
3:00 – 6:00 usiku | Tuzo za fainali na Burudani |
SHERIA ZA MATUMIZI YA KAMERA:
- Hakuna mpiga picha na video atakeye ruhusiwa kuchukua matukio yeyote.
- Hairusiwi kwa mtu yeyote kuchukua matukio ndani ya eneo la shughuli.
- Hairusiwi kupiga picha kwenye jukwaa
Maelekezo yote hapo juu yatatolewa na Pilipili Ent. Productions