(255) 0753559833

Nidhamu Yetu

Mr. Tanzania :

Mwanamichezo anafanya mazoezi ya kujenga mwili wote na wenye uwiano sawa.Kila kiungo kikiwa katika muonekano ulio sawa bila kuzidi kiungo kingine hakutakiwi kuwa na sehemu ya mwili yenye kuonekana dhaifu au msuli ambao umejengwa katika kiwango cha chini,badala yake wanatakiwa kufuata mpangilio maalumu wa mazoezi ya awali ya kabla ya shindano,pia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiwango cha chini kabisa.Kuondoa maji ambayo yako chini ya ngozi ili mwili uonekane kuwa mkavu na kuonyesha kiwango cha ubora wa misuli,ukubwa,ujazo,mgawanyiko na mikato.Yule ambaye ataonyesha misuli ambayo itaonekana kwa ufasaha ndiye atapata alama za juu katika shindano.Na kingine kikubwa kinachotazamwa kwa umakini ni muonekano mzima wa mwili ulio na uwiano sawa .Hii inamaanisha kwamba mabega mapana na kiuno chembamba miguu yenye ujazo na umbo la juu lenye muonekano mzuri .Muonekano wa aina hiyo utaonyeshwa wakati wa mzunguko wa kwanza wakati wa kuwachunguza washiriki kwa umakini mbele ya waamuzi wa mashindano na ambapo watakapokuwa wanafanya onyesho la kutanua misuli kwa kutumia mitindo saba ya msingi ya utunishaji misuli wakati wa shindano,washiriki watatu hadi wanne ambao watateuliwa na waamuzi,washiriki wanapanda katika onyesho wakiwa wamevaa vazi maalumu fupi kwa ajili ya maonyesho ya mwili mzima na pia miguuni wakiwa watupu wakiwa bila viatu pia katika shindano kuna mzunguko ambao washiriki wanapewa sekunde sitini kuonyesha misuli yao huku wakifuata midundo ya muziki wa chaguo lao binafsi. Ni aina ya mtindo wenye kuvutia wa kisanii zaidi,mitindo ya msingi ya utanuaji misuli na ile ya kawaida hutumiwa na washindani katika kuonyesha na kutanua misuli kwa kutumia muziki,Kunakuwa na mizunguko mitatu katika kila mzunguko kila mwamuzi lazima amuweke sawa mshindani ili apate kumtazama kwa umakini zaidi huku wakiwapa nafasi sawa ya kuonekana kutoka Yule wa kwanza hadi mwisho katika mstari.

Mr. Physique :

Ni aina ya Shindano ambalo wale wajenzi wa mwili wa kiume wasiopenda kujenga misuli ya mwili kwa kiwango cha  juu lakini wanapenda kuwa na misuli ya kiwango cha kawaida lakini yenye kupendeza,

Ili kuweka fursa sawa kwa wote ,Washiriki wanashindanishwa kulingana na urefu wa maumbo yao,kwa kufuata mfumo maalumu wa Shirikisho la kujenga Mwili Tanzania(TBBF) Kila ngazi ya ushiriki na daraja lake,kwa sasa kuna madaraja ya ushindani matano ambayo ni kwa urefu wa umbo 168cm,171cm,175cm,180cm na zaidi ya 180 cm)

Ikiwa suala la ukubwa wa misuli si suala la msingi sana katika mwili wa mashindano katika daraja hili la ushindani kinachotazamwa kwa umakini zaidi ni jinsi gani mwili ulivyojengeka kwa uwiano ulio sawa,umbo la msuli na kiwango cha mafuta cha chini,mikatiko na migawanyiko ya misuli, Viwango hivi huangaliwa kwa umakini na waamuzi wa shindano wakati wa mzunguko wa 1na wa 3,katika mzunguko wa 2 pia ,kama ilivyo katika shindano la ujenzi wa mwili pia vile vile katika shindano hili pia kuonyesha mitindo ya utanuaji misuli inatumika kwa kufuata mapigo ya muziki anaochagua mshindani.

Ms. Fitness :

Hili daraja la ushindani litathibitika kuwa la umaarufu zaidi. Shirikisho la ujenzi wa mwili Tanzania limeongeza kiwango cha madaraja ya ushindani katika kundi hili na kuwa la makundi manne tofauti ya urefu wa 170cm.174cm.178cm. na zaidi ya 178cm. Wao watafanya mizunguko miwili ya kugeuka kushoto na kulia huku wamevalia kaptula fupi za pendekezo lao wenyewe. Mzunguko wa  pili ambao utakua ndio fainali ya shindano lao litaruhusu kila mshiriki kupanda jukwaani akiwa peke yake akitazamwa muonekano wake kwa ufasaha. Shindano hili lengo lake ni kwa ajili ya wasichana ambao wanafanya mazoezi ya gym kwa ajili ya kuweka maumbo yao vizuri pia wanakula   chakula kwa kufuata mpangilio mzuri,lakini ambao wanapenda kujenga mwili. Kwa wakati huo huo wakiwa na umbo zuri lenye kupendeza.Ni washindani ambao wanaonekana kuonyesha umbo lililo kamilika na lenye uwiano sawa lililochanganyika na misuli na ukakamavu.Washindani wa shindano hili wanahitajika kuwa na muonekano wenye hadhi na kujiamini kwao kuwe kwa uwazi kabisa.