(255) 0678 393 950, 0753559833

Utangulizi

Shirikisho la ujenzi wa mwili Tanzania (TBBF) kwa ushirikiano na PILIPILI ENTERTAINMENT COMPANY LIMITED wanapenda kuutangazia uma uzinduzi wa mashindano ya ujenzi wa mwili ya Mr Tanzania. Mashindano ya ujenzi wa mwili ya Mr. Tanzania yatawaleta pamoja watunisha misuli hodari toka Tanzania nzima bara na visiwani kushindania taji lenye hadhi la “Mr. Tanzania”. Kilele cha mashindano ya Mr. Tanzania kitapangwa kufanyika Dar es salaam tarehe November 2018. Mshindi wa mashindano ya Mr. Tanzania ataiwakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya wajenzi wa mwili ya Mr. AFRICA, MR. UNIVERSE, na MR. WORLD yatakayofanyika Novemba 2019.

Wajenzi wa mwili tu ambao ni wazawa na raia wa kujiandikisha bila kubagua rangi, dini wala kabila wana ruhusiwa kushindania taji lenye hadhi la Mr. Tanzania

Mr. Tanzania 2018 itaandaliwa kiutalaamu na wandaaji bora kabisa wa maonesho kwenye hii tasnia. Pilipili entertainment Company Limited wamepewa kibali kama waandaaji rasmi wa kulisimamia hili tukio na watachukua picha za filamu za mwenendo mzima wa washiriki kwa wakati muafaka toka mikoa yao na majiji yao pia na gym pamoja na mkufunzi kwa ajili ya washiriki. Hii itatengenezwa kuwa kipindi cha kwenye runinga na kuoneshwa kama tukio kwenye runinga moja ya Taifa kuanzia siku ya kwanza washiriki wakianza mazoezi yao mpaka siku ya kilele ambayo itaonehswa moja kwa moja kwenye chaneli ya ITV.

Tuna mataji matano tofauti ya kushindaniwa kwenye ngazi ya Taifa ukiachana na tukio lenyewe la taji lanyewe la Mr. Tanzania ambalo litakuwa ngazi ya kimataifa, ambayo ni:

  1. Miss Fitness 2018
  2. Mr. Photogenic 2018
  3. Mr. Handsome 2018

Mataji yote hayo yapo wazi kushindaniwa na watu binafsi bila kujiunga na gym. Haya mataji yatawaleta kwenye mwonekano wale wenye hamasa ya kuwa wana mitindo, wasanii au kwa kutaka kuwa maarufu nchini. Haya mataji pia yanafungua fursa nyingi kwa washiriki kwenye tasnia ya filamu na matangazo ya kwenye runinga kama wasanii, na TBBF kwa kushirikiana na Pilipili entertainment company Ltd ambao ni wakongwe kwenye hii tasnia watawasimamia hawa washindi chini ya mpango wa usimamizi kwa kipindi cha miaka 3 kwa kuongeza ubora kwenye kazi yao.