(255) 0678 393 950, 0753559833

Frequently Asked Questions (FAQ)


Hatua zipi za kufuata ili kujiandikisha katika shindano la ujenzi wa mwili la Mr. Tanzania 2017 ?

Kama Ni Mshiriki Wa Binafsi Kuwezi Kujiandikisha Mwenyewe Yakupasa Kujisajili Kupitia Katika GYM Yako Au Health Club Unayofanyia Mazoezi. Hii Ina Maanisha Kwamba GYM Au Health Club Yako Ndio Wanakuwa Wadhamini Wako Katika Mashindano


Je, Ni Hatua Zipi Zinatakiwa Kufuatwa Ili Kujiandikisha Katika Shindano La Mr. Handsome?

Katika shindano hili unaweza kujiunga kama mtu binafsi kupitia tovuti yetu nenda moja kwa moja katika “mashindano” katika menyu kisha bonyeza “Mr. Handsome Registration Form” na kisha jaza fomu, pia usisahau kuambatanisha na picha 4-7 katika mkao wa mwonekano tofauti ulio oneshwa katika fomu yako ya kujiunga, picha zikiwa katika kiwango cha juu cha ubora, pia usipake mafuta mwili wako kwa wingi wakati wa kupiga picha, paka kwa mbali tu, na pia hutakiwi kujipaka rangi zozote mwilini mwako wakati wa upigaji wa picha. Baada ya kuwasilisha fomu yako unatakiwa kulipia ada yako ya kujiandikisha katika shindano kupitia mfumo wa malipo ulio orodheshwa kwenye fomu yako kama vile ulivyooneshwa TIGOPESA Namba 0678 393950, MPESA 0753 559833, au unaweza peleka benki kupitia Ankara/ taslimu katika benki ya EQUITY namba ya akaunti ni 3007211301051, jina la akaunti ni Tanzania body building federation. Ukishamaliza kufanya malipo utatuthibitishia kuwa tayari umekwisha fanya malipo kwa kututumia ujumbe mfupi wa simu wa uthibitisho uliyopokea toka tigopesa au mpesa katika namba za simu au kama umelipa kwa kutumia Ankara basi tuma na risiti kivuli ya benki uliyotuma na kututumia kupitia barua pepe yetu, barua yetu pepe ni info@tzbbf.com au unaweza tuma uthibitisho wa malipo kwa ujumbe wa simu ya mkononi kupitia namba zilizopo hapo juu, au kwa njia ya whatsapp kupitia namba hizo


Je, Ni Hatua Zipi Zinatakiwa Kufuatwa Ili Kujiandikisha Katika Shindano La Mr. Photogenic?

Katika shindano hili unaweza kujiunga kama mtu binafsi kupitia tovuti yetu nenda moja kwa moja katika “mashindano” katika menyu kisha bonyeza “Mr. Photogenic Registration Form” na kisha jaza fomu, pia usisahau kuambatanisha na picha 4-7 katika mkao wa mwonekano tofauti ulio oneshwa katika fomu yako ya kujiunga, picha zikiwa katika kiwango cha juu cha ubora, pia usipake mafuta mwili wako kwa wingi wakati wa kupiga picha, paka kwa mbali tu, na pia hutakiwi kujipaka rangi zozote mwilini mwako wakati wa upigaji wa picha. Baada ya kuwasilisha fomu yako unatakiwa kulipia ada yako ya kujiandikisha katika shindano kupitia mfumo wa malipo ulio orodheshwa kwenye fomu yako kama vile ulivyooneshwa TIGOPESA Namba 0678 393950, MPESA 0753 559833, au unaweza peleka benki kupitia Ankara/ taslimu katika benki ya EQUITY namba ya akaunti ni 3007211301051, jina la akaunti ni Tanzania body building federation. Ukishamaliza kufanya malipo utatuthibitishia kuwa tayari umekwisha fanya malipo kwa kututumia ujumbe mfupi wa simu wa uthibitisho uliyopokea toka tigopesa au mpesa katika namba za simu au kama umelipa kwa kutumia Ankara basi tuma na risiti kivuli ya benki uliyotuma na kututumia kupitia barua pepe yetu, barua yetu pepe ni info@tzbbf.com au unaweza tuma uthibitisho wa malipo kwa ujumbe wa simu ya mkononi kupitia namba zilizopo hapo juu, au kwa njia ya whatsapp kupitia namba hizo


Hatua zipi muhimu za kufuata ili kujiandikisha kwenye shindano kwa mshiriki katika shindano la Mr. Tanzania?

Katika shindano hili, GYM na klabu za mazoezi ndizo huchagua watu wao wa kushiriki shindano, ujiandikishaji wa mtu binafsi hauruhusiwi, ili uweze shiriki shindano ni lazima uwe mwananchama wa GYM husika ndipo upate ruhusa na Baraka za kushiriki, nenda katika neno “Mashindano” kasha nenda katika menyu ya juu na bonyeza neno “Mr. Tanzania” na kasha ujaze fomu. GYM na klabu zitajaza maelezo yake katika kuelezea mahali ilipo na jinsi vile ilivyoanza na washiriki wao walio wateua kushiriki shindano kama wawakirishi wa gym ukihusika katika maandalizi ya mshiriki, kila gym iko huru kuteua wawakilishi wao katika shindano katika idadi wanayotaka wao ambao watawasaidia katika maandalizi ya kujiandaa na shindano ila watachajiwa kwa ajli ya ushiriki wa washiriki wawili tu, iwapo kama kutakuwa na washiriki zaidi ya wawili ambao wanashiriki shindano basi ada ya malipo yako ya mwaka itakuwa ni shilingi 100,000 imeongezeka, hii ina maana kwamba unalipa ada ya shilingi 200,000 na unaruhusiwa kuingiza washiriki wengine wawili bure kwa gharama hiyohiyo uliyotoa, iwapo kama kutakuwa na ongezeko zaidi la washiriki kutoka katika gym yako itabidi kila mshiriki aliezidi kulipiwa shilingi 100,000 baada ya kujaza hati hii au fomu bila kubakiza chochote au nafasi yoyote yakupasa kubonyeza neno “Wasilisha” usisahau kuambatanisha za kiola mmoja wa washiriki wako ambazo ni 4-7 katika mikao tofauti tofauti ya utunishaji misuli kama ulivyooneshwa katika hati ya uanachama zikiwa katika kiwango cha juu cha ubora, mwili wako usiupake mafuta sana wakati wa upigaji wa picha. Baada ya Skuwasilisha hati hii unatakiwa kulipa ada ya ushiriki kupitia mfumo wa wa malipo ulio orodheshwa kwenye fomu yako kama vile ulivyooneshwa. TIGOPESA Namba 0678 393950, MPESA 0753 559833, au unaweza peleka benki kupitia Ankara/ taslimu katika benki ya EQUITY namba ya akaunti ni 3007211301051, jina la akaunti ni Tanzania body building federation. Ukishamaliza kufanya malipo utatuthibitishia kuwa tayari umekwisha fanya malipo kwa kututumia ujumbe mfupi wa simu wa uthibitisho uliyopokea toka tigopesa au mpesa katika namba za simu au kama umelipa kwa kutumia Ankara basi tuma na risiti kivuli ya benki uliyotuma na kututumia kupitia barua pepe yetu, barua yetu pepe ni info@tzbbf.org au unaweza tuma uthibitisho wa malipo kwa ujumbe wa simu ya mkononi kupitia namba zilizopo hapo juu, au kwa njia ya whatsapp kupitia namba hizo


Je, nitajuaje kama nimechaguliwa au sijachaguliwa?

Mara tutakapo pata malipo uliyolipa tutakutumia uthibitisho wa malipo yako kupitia barua yako pepe na ndipo taarifa na kila kitu vitatangazwa kupitia tovuti yetu pia magazetini, radio na Runinga, pia utajulishwa moja kwa moja kupitia anuani yako ya barua pepe.


Ni vipi kama sijachaguliwa, Je ntapata fidia ya pesa yangu?

Hapana! Mara tu utakapokuwa umejaza hati ya ushiriki wa shindano na kuambatanisha picha zako kabla ya tarehe 28 April 2017 ndipo waamuzi wetu wa shindano watazichambua picha na kasha kuchagua washiriki ambao wataingia hatua ya awali ya mchujo itakayofanyika Dar es salaam, washiriki ambao watakuwa wamechaguliwa kupitia katika mtandao kupitia picha zao watapewa kati ya tar 26 au 27 mwezi wa kwanza kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hatua ya awali ya mchujo, wengine wote ambao watakuwa wamekosa kuchaguliwa watajulishwa kuhusu kutochaguliwa kwao pia watarudishiwa pesa zao ndani ya siku 90 baada ya malipo yao kukatwa aslimia 10 kwa ajli tu ya gharama za marejesho, malipo ya kurudishiwa pesa ndani ya siku 90 yatafanyika kwa washiriki wa Mr Handsome bodybuilder na Mr Photogenic bodybuilder pekee, kukatwa asilimia 10 kwa mshiriki baada ya kurudishiwa pesa maana yake kama umelipa 50,000 kwa ajili ya ushiriki, iwapo haujachaguliwa itabidi urejeshewe shilingi 45,000

Pia iwapo kama washiriki watakuja Dar es salaam kibinafsi tar 26 na 27 May, iwapo kama hawakuchaguliwa kwa ajili ya kuingia fainali ya shindano la Mr. Tanzania mwezi December 2017. Pesa zao hawatarudishiwa!


Ni nini kitafuata baada ya mimi kuchaguliwa katika hatua za awali ?

Mara utakapokuwa umechaguliwa katika hatua za awali tarehe 26 na 27 Januari 2017 utaombwa ubaki siku mbili nyingine zaidi Dar es salaam. Katika siku mbili ambazo utakuwa umebaki Dar es salaam utatambulishwa katika nchi nzima kupitia vyombo vya habari, utahudhuria kikao na waandishi wa habari, tutakuwa na mwongozo wa ana kwa ana na mshauri wa mambo ya mazoezi toka shirikisho la ujenzi wa mwili (TBBF)katika kujua mambo mbalimbali ya ujenzi wa mwili na mengineyo. Pia utakutana na watayarishaji toka kampuni ya mambo ya burudani Pilipili entertainment company limited ambao watawaelezea washiriki na wawakilishi wa gym zao jinsi gani tukio litakavyooneshwa kwenye runinga kama kipindi maalum cha maonesho halisi (reality show)


Onesho hilo halisi linahusu nini ?

Lishando lote la ujenzi wa mwili litachukuliwa moja kwa moja kama kipindi, moja kwa moja tangu hatua za awali kabisa na kampuni ya Pilipili Entertainments mpaka siku ya fainali yenyewe ya shindano tarehe December 2017.

Waandaaji wa shindano na kipindi watatembelea mkoa/jiji na katika gym yako kuangalia jinsi unavyoendelea na maandalizi ya shindano kila mwezi, mtangazaji wa kipindi ataongea na wewe kuhusiana na maandalizi yako magumu ya shindano. Haya yote yatafanyiwa uhariri wa kuoneshwa katika kituo cha Televisheni ya Taifa kila ijumaa na jumamosi au kila siku kwa dakika chache itategemeana na upenzi wa wa wananchi wa Tanzania watakavyokipokea kipindi na jinsi kitakavyokuwa kikisonga mbele.


Nini faida ya GYM kuwa mwanachama wa shirikisho la kujenga mwili (TBBF) ?

Mbali na kupata ushindi wa pesa tasilimu, iwapo GYM inakuwa imetoa mshindi wa shindano kuna fursa kubwa zaidi ya GYM kujiunga nasi:

  1. Bila kujihusisha na gym mshiriki hawezi shiriki shindano la Mr. Tanzania, hii inamaanisha kwamba Gym ndio inabeba wajibu wa kuwa kama shirikisho iwapo mshiriki atapenda kushindana, nah ii inaipa GYM wanachama wengi kuja kufanya mazoezi
  2. GYM inapata kujitangaza tangu siku ambayo washiriki wake wanakuwa wameingia katiika mchujo wa awali wa mashindano kupitia mitandao ya kijamii, runinga na radio, hii ina maana ni matangazo kwa kiwango cha juu kwa GYM yako
  3. GYM itakuwa na lengo na sababu ya kuandaa na kuwasaidia washiriki wa maandalizi ya mashindano na hii italeta changamoto kubwa ya ufanyaji mazoezi kwa wanachama wako, kuwafanya wahamasike na hali ya kiushindani ndani ya GYM
  4. Mwakilishi mmoja toka katika GYM yako atapata fursa ya kuwasindikiza washiriki kuja katika mchujo wa awali na siku fainali yenyewe ya mashindano katika jiji la Dar es salaam
  5. Mfumo huu utaongeza utamaduni wa watu kupenda mazoezi ya GYM na GYM nyingi zitapata faida kubwa
  6. Chini ya mwamvuli wa uongozi wa shirikisho la ujenzi wa mwili Tanzania wenye gym zao watapata kusikilizwa sauti zao pale itakapohitajika, kutakuwa na matukio kadhaa makubwa katika mwaka yatakayoendeshwa na shirikisho la kujenga mwili Tanzania (TBBF) ambayo yataleta faida kubwa katika GYM husika iwapo zitakuwa mwanachama wa shirikisho la kujenga mwili Tanzania, matukio kama vile afya na ukakamavu kwa ajili ya watoto, wanawake na wazee, wanaume na wanawake yatafanyika kwa mashindano yao pekee
  7. Kupata ushauri wa bure kiufundi kwa wataalamu waliobobea katika maswala ya mambo ya mazoezi ya ujenzi wa mwili, kuhusiana na vifaa gani muhimu ndani ya GYM, pia kujua bidhaa na mambo mengi yanayohusiana na ujenzi wa mwili wenye afya bora.

Ni nani atahusika na gharama za matumizi na gharama zote wakati wa kuingia na kutoka katika tukio la mchujo wa awali na mpaka siku ya fainali kuu?

Gharama zote za usafiri wa washiriki na wawakilishi wao zitabebwa na wao wenyewe, usafiri na malazi utakuwepo tu kwa wale ambao watakuwa wamechaguliwa katika mchujo wa awali na kwa ajili ya fainali kuu zitagharamiwa na shirika lenyewe.