(255) 0753559833

Ujumbe Toka Kwa Mwenyekiti

Wapendwa Wajenzi wa Mwili na Wadau wa Mazoezi ya kujenga Mwili Tanzania,

Kwa niaba ya Shirikisho La Kujenga Mwili Tanzania (TBBF)Nina furaha kubwa kuwakaribisha katika Tovuti Yetu Maalumu ,

Shirikisho La Kujenga Mwili Tanzania Likiwa limeanzishwa mnamo mwaka 1996 na Fike Wilson ambae ni mshauri wa mambo ya ufundi wa maisha katika masuala Mchezo wa ujenzi wa Mwili Tanzania na utunishaji wa Misuli, Sasa Wadau wake watapata taarifa mbalimbali kuhusiana na masuala ya ujenzi wa mwili na kuhusiana na habari za mchezo wa kutunisha misuli kupitia Tovuti yetu t.b.bf.com, Habari zote muhimu za mashindano Nchini Tanzania zitawafikia mamia ya mashabiki na wadau watazipata kupitia Tovuti yetu,Historia ya Mashindano ya Kujenga Mwili na kuhusu matukio yanayotokea katika mchezo wa kujenga mwili,Pia kujua sheria za mchezo wa kujenga mwili,vile vile kujua habari za Mashindano yanayosimamiwa chini ya nembo ya Shirikisho la kujenga Mwili Tanzania, Wadau na Mashabiki wa Mchezo wa kujenga Mwili Tanzania, Wadau na Mshabiki wa mchezo wa kutunisha misuli na ujenzi wa mwili Nchini Tanzania na Duniani pote kwa ujumla tunaungana na wote kwa pamoja kupitia mtindo wa maisha wa kujenga mwili na mchezo wa kujenga na shauku kuu ya kufanya mazoezi ili kuwa na afya njema,Ujenzi wa Mwili unakuwa mchezo pale mjenzi wa mwili anapokuwa amejenga mwili kwa kiwango cha kufikia kuwa na hamu ya kutaka kushiriki mashindano ya kujenga mwili,

Shirikisho la kujenga Mwili Tanzani liko mbioni katika kufanya mapinduzi kuinua msisimko wa mashindano ya ujenzi wa mwili Tanzania, kwa jinsi mashindano ya kujenga mwili yatakavyochukuliwa kwa umakini mkubwa katika kipindi hiki kutakuwa na uchukuaji wa matukio yatakayochukuliwa moja kwa moja na wataalamu wa uchukuaji wa picha za filamu toka kampuni ya matangazo ya biashara na filamu ya PILIPILI ENTERTAINMENT hatua kwa hatua hadi kuelekea siku ya fainali ya Mr Tanzania na pia wandaaji wa mashindano wanatarijia kufanya vile iwezekanavyo kufanya mashindano ya Mr Tanzania kuwa yenye msisimko wa ajabu na kiwango cha juu zaidi na pia kuhamasisha vijana wajenzi wa mwili kujiunga kwa wingi katika mchezo huo kwa miaka mingi ijayo na kuufanya ujulikane zaidi na zaidi nchini Tanzania

Shirikisho la ujenzi wa mwili Tanzani a lina mahusiano na utendaji wake kikazi na baraza la michezo la taifa (BMT), COSOTA pia shirikisho la ujenzi wa mwili duniani (IFBB) na pia kwa ajili ya kuwainua washindani wa ujenzi wa mwili na kuwapeleka katika mashindano makubwa kimataifa, na hivi karibuni tutambulika na kamati ya taifa ya Olimpiki pia na kujiunga na taasisi ya Dunia ya upingani wa matumizi ya madawa ambayo itafanya kuwa shirikisho la ujenzi wa mwili Tanzani kuwa shirikisho lenye mamlaka makubwa katika ujenzi wa mwili na katika vita katika kupambana na matumizi ya madawa katika michezo (WADA)

Shirikisho la ujenzi wa mwili litakuwa na ushirikiano wa karibu wa kisayansi na mashirikisho ya kimataifa, ikiwa inajua umuhimu wa faida ya ujenzi wa mwili katika kutengeneza afya ya wananchi wengi kwa ujumla kupitia mazoezi ya ujenzi ya mwili ambayo yamekuwa yakizuia kuzeeka kwa haraka kwa wafanya mazoezi ambapo kwa mfano mzuri ni pale wajenga mwili wenye umri mkubwa kuanzia zaidi ya miaka 50, 60 na 65 wanashindana katika mashindano ya ujenzi wa mwili

Matukio ya kimichezo ambayo yatajumisha wanamichezo vijana na kujumuisha watoto pia katika kuwaweka katika hali ya afya njema na ukakamavu yatapewa kipaumbele cha juu zaidi siku za mbeleni

Tunafurahi kuwaletea taarifa zote muhimu kuhusiana na ujenzi wa mwili kwani ujenzi wa mwili ni shauku ya kukufanya kuwa na afya njema na maisha yenye uchangamfu na furaha

Wako katika Michezo

Mwenyekiti wa Shirikisho ra kujenga mwili Tanzania

Amri Jonah