Language:

 • Swahili
 • English
(255) 0678 393 950, 0753559833

Tuzo Za Kushindaniwa

SHINDANO LA MR. TANZANIA

TUZO KWA MSHINDI WA MR. TANZANIA 2017

 1. Kombe zuri la kupendeza la “Mr. Tanzania 2017” beji maalum na cheti cha ushiriki wa shindano
 2. Mshindi wa “Mr. Tanzania body builder” atazawadiwa shilingi milioni 10 pamoja na gari
 3. Udhamini wa kutosha kwa ajili ya maandalizi ya kuiwakilisha nchi ya Tanzania katika shindano la Mr. Afrika akiwa na bendera ya Tanzania
 4. Mshindi aliepata kushinda taji la Mr. Afrika ataletwa ilia je asaidie kushauri na kumpa mazoezi mshindi wa shindano la Mr. Tanzania
 5. Miaka mitatu ya usimamizi kimkataba pale ambapo mshindi atakapotangazwa na kutumika kwa ajiri ya matangazo ya biashara na kumtangaza yeye binafsi
 6. Na pia tunzo zingine pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wa mchezo

 

TUZO KWA MSHINDI WA PILI WA MR. TANZANIA 2017

 1. Mshindi wa pili wa Mr. Tanzania 2017 atazawadiwa kikombe cha ushindi wa pili, Beji maalum, cheti cha ushiriki, shilingi milioni 5
 2. Mkataba wa miaka mitatu kwa chini ya usimamizi ambapo mshindi wa pili atasaidia katika mambo ya mikataba ya biashara na matangazo

 

TUZO KWA MSHINDI WA TATU WA MR. TANZANIA

 1. Mshiriki wa tatu wa taji la Mr. Tanzania 2017, kikombe, Beji maalum, cheti cha ushiriki na
 2. Zawadi ya shilingi milioni 2 na nusu tu (Tsh 2.5m)
 3. Mkataba wa usimamizi wa miaka mitatu pia kutangazwa kwa ajili ya matangazo ya kibiashara

 

TUZO KWA MR. TANZANIA HANDSOME 2017

 1. Kombe zuri la “Mr. Tanzania most handsome 2017 na cheti cha ushiriki wa shindano
 2. Mshindi atazawadiwa shilingi milioni 5 (Tsh 5m)
 3. Mkataba wa usimamizi wa miaka mitatu kwa ajili ya kutangazwa, pia kufanya matangazo ya biashara
 4. Na zawadi nyingi kutoka kwa wadhamini na wadau wa michezo
 5. Mkataba wa kufanya filamu/ mchezo wa kuigiza katika runinga kutoka waandaaji wa shindano la Mr. Tanzania 2017 PIlipili entertainment company kwa kuvaa uhusika mkuu wa filamu/ mchezo wa kuigiza katika runinga.

 

TUZO KWA MR. TANZANIA PHOTOGENIC 2017

 1. Kombe zuri la ushindi na cheti cha ushiriki
 2. Mshindi atazawadiwa shilingi milioni tano( Tsh 5m)
 3. Mkataba wa miaka mitatu kuwa chini ya usimamizi kwa ajili ya kutangazwa kufanya mikataba ya kibiashara
 4. Na pia zawadi nyingi toka kwa wadhamini na wadau wa mchezo, pesa taslimu pia
 5. Mkataba wa kufanya filamu/ mchezo wa kuigiza katika runinga toka kwa waandaaji wa shindano, Pilipili entertainment, ukivaa uhusika mkuu

 

TUZO KWA GYM BORA TANZANIA

 1. GYM/ HEALTH CLUB itakayotoa mshindi wa shindano la Mr Tanzania 2017 kutokana na kumsaidia mshindi kushinda shindano kwa kumpa msaada wa hali na mali hadi kufikia ushindi. GYM/ HEALTH CLUB itazawadiwa zawadi ya tunzo ya GYM bora zaidi Tanzania, pia pesa taslim milioni tano, kikombe cha ushindi, beji maalum na cheti cha ushiriki
 2. Vilevile kwa GYM itakayotoa mshindi wa pili itapata Tsh 2.5M, kikombe, beji na cheti cha ushiriki
 3. GYM/ HEALTH CLUB itakayokama nafasi ya tatu itapata shilingi milioni 1

Tafadhali soma hapa:

Tuzo zote za pesa na mataji yanahusiana na makato ya sheria za mamlaka ya mapato Tanzania